Wednesday, April 24, 2013

WATANZANIA KWA KUPENDA SIFA.

Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya walikamatwa na madawa ya kulevya China. Wakaambiwa adhabu ni mbili kifo au adhabu nyingine ambayo wakiishindwa pia wanauawa. Wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao. Wakapelekwa msituni wakaambiwa waingie msituni kila mmoja kwa njia yake halafu kila mmoja arudi na matunda kumi ya kufanana. Wakaingia msituni kila mtu njia yake. Mnyarwanda akarudi wa kwanza. Karudi na maepo kumi. Akaambiwa adhabu ni kuyameza yote mazima mazima moja baada ya jingine bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Wa pili Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogoo. Kumi. Vya kufanana. Vidogo kama pipi. Akaambiwa masharti. Akaanza kula bila kufumbua macho wala kulia wala nini. Alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa. Wakiwa kuzimu Mnyarwanda akamuuliza Mkenya.. "Vipi wewe mbona ulishindwa kuvumilia wakati ulibakisha kitunda kimoja tu?" Mkenya akajibu: "Kaka, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mtanzania anakuja na matikiti maji!".....

No comments:

Post a Comment