Wednesday, April 24, 2013

KWA WANAWAKE WENYE AKILI, KAMA HUNA AKILI USISOME

Kama kuna mwanaume amekuacha bila sababu yoyote ya msingi,au ametafuta kasababu ka kijingajinga tu ili abreak up,amepata mwanamke mwingine.Ukaumia,ukalia,ukapona,ukapata mtu mkaanzisha mbingu yenu yenye amani na raha,GHAFLA yule furushi aliyekuacha anaanza kurudi,mara akosee message, atume kwako,mara anajikomba kuomba msamaha kurudi baada ya kuona kule mambo sio,eti shetani alimpitia,kwani siku hizi Shetani ana gari hadi ampitie yeye tu?KAMWE usilambe matapishi.
Usikubali kugeuzwa ARV,vile vidonge,ili umuongezee maisha yeye baada ya kukumbana na virusi vya kuachika huko alikokimbilia kwa mbwembwe.Mwanaume ni msimamo,kama alikuacha kwa sababu,ukikubali kumrudia tena ipo siku atapata sababu tena ya kukuacha na utaumia mara mbili...

No comments:

Post a Comment