Friday, February 15, 2013

am ok! mengine yapo moyoni

imezoeleka katika jamii unapomuuliza hali jirani yako anakujibu SIJAMBO wakati maskini ana matatizo na mambo kibao yanayo mzunguka ambayo yanamnyima utulivu wa nafsi na akili yake, hata anapopata maudhi utamuona ni mjasiri akionekana hamna tatizo lililompata. Wakati mwingine anapokuwa na huzuni utamuona hatoi chozi kumbe moyoni analia.just because my eyes dont tear doesnt mean my heart doesnt cry..laiti ungeweza kuungalia moyo nini unahisi na wewe ungelimuonea huruma.

enjoy a little thing

hata kile kidogo ulichokuwa nacho ni vema ukaridhika nacho nacho na kukifurahia kwa sababu wapo ambao wanahitaji kama chako na hawakipati. Fahamu kwako ni kidogo kwa wengine ni kikubwa na kile unachokiona kwa mtu ni kikubwa basi fahamu upo uwezekano mkubwa sana na yeye kwake ni kidogo..hivyo basi thamini madogo unayoyafanya sasa kwani baadae ni mambo makubwa na yatakupatia kumbukumbu nzuri na mafunzo kadri ya muda unavyozidi kwenda..you can enjoy a little thing because one day you will realize they were a big thing, ridhika na ulichonacho hata kama ni kidogo kama sisimizi.

dont cheat to a good person

kuna wakati unapokutana na marafiki, ndugu au jamaa ni vema ukatambua thamani yao na sio kuwachukulia wote katika nafasi na viwango sawa kwa sababu unaweza ukampoteza mtu ambaye ni mzuri na muhimu sana kwako, hasa pale unapozingatia umemuongopea kwa kumdanganya na hata kukaribia kumdhulumu kwa kumpotezea muda na uaminifu juu yako..cheating on a good person is like throwing away a diamond and picking up a rock..jitahidi kuishi vizuri na rafiki, ndugu, jamaa au jirani yako kwa wema