Friday, May 3, 2013

TANGAZO, Mtu mwenye watoto 10 atazawadiwa mil 50;

 Jamaa baada ya kusikia tangazo akamwambia mke wake, sisi tuna watoto 9, ila nikwambie mke wangu mimi nina mtoto 1 nje ya ndoa, naomba tumchukue na huyo wawe 10 tupate hizo ml 50. Mkewe akamwambia poa. Jamaa akaenda kumfata huyo mtoto. Aliporudi hakuwaona wale 9. Akamuuliza mkewe, Watoto wako wapi? Mkewe akajibu, baba zao walipoona tangazo nao wamekuja kuchukua watoto wao, Jamaa akazimia.....!!

USINGIZI MTAMUU

Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe.Mara akamuona mtu amesimama kitandani.
Jamaa akafoka,"Toka hapa,we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?                                      " Yule mtu akajibu,"Mi ni malaika;mtakati fu petro,na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!"
Jamaa,"Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijana...naomba nirudishwe!"
Malaika,"Inawez ekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku."
Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda,akaonel ea arudi kama kuku.
Malaika akamgeuza kuku,akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.
Akachuchumaa na kuanza kujikamua;yai la kwanza likatoka.akajik amua tena,yai la pili likatoka. Akajik amua tena mara ya tatu.
Wakati yai la tatu linatoka...akas htukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, "Pumbavu! Balaa gani hii....unakunya kitandani!

HAHAHAHA KAMA NI WEWE UNGEFANYA NINI?

Jamaa mmoja alipata mchumba akaona ni vyema amtambulishe kwa baba yake, mzee alipomuona tu akasema, "oho huyu ni dada yako ni mtoto wangu huyu nilizaa kipindi niko shule", jamaa akatafuta mchumba mwingine akafanya vile vile lakini mzee akasema "oho ulimufahamu vipi huyu ni dada yako pia" jamaa akaona isiwe shida akatafuta kimwana mwingine, digi alipopelekewa na huyo akasema "aha sasa ww mtoto kwanini unakuwa unakutana na dada zako tu, huyu naye ni dada yako tafuta mwingine ila usimwambie mama yako maana hajui kama nina watoto hawa", 
jamaa akawa na hasira sana akaenda kumpatia story yote mama yake, mama akamwambia "aha hata usijali hao sio dada zako hata kwa damu maana hata wewe huyu sio baba yako ila usimwambie maana hajui ni siri yangu ya muda mrefu, wewe fanya kuchangua unayempenda kati ya hao uoe.

UROHO M-BAYA..

Mwizi alibomoa nyumba akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye kibakuli vilivyokauka,akaonja kimoja akaona ni kitamu kina chumvi chumvi! Akafurahi akakaa chini akala vyote alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa CHUMBA CHA KUTAHIRIA!! eti unahisi alikula nini?

KWA KUPENDA SIFA.

Wahaya kwa kupenda sifa! leo katika matangazo ya vifo , ndugu Deus Rweyemamu wa masaki anasikitika kutangaza kifo cha mwanawe Joseph Rweyemamu wa Oysterbay, kilichotokea jana Australia baada ya kupaliwa na baga akiwa anaendesha hummer yake mpya. Msiba utafanyika kwa anti yake marekani, taarifa zimfikie Ronaldo Rweyemamu wa Portugal, Koku Kardashian Rweyemamu wa U.S.A, Torres Rweyemamu wa Spain, Walcot Rweyemama wa England, na house girl wao alioko Dubay katika shoping ya mwezi, akamalizia tutawasiliana baadayeeee.

ZIMA MZIKI

Jamaa alipanda tax akamwambia dereva, zima mziki dini hairuhusu kuckliza nyimbo za kidunia kwa sababu wakati wa Yesu hapakuwa na redio, dereva akatii akazma halaf akasimamisha gari na kufungua mlango wa abiria. Jamaa akamuuliza Nini tena? Dereva akajbu 'wakati wa Yesu hakukuwa na tax shuka usubiri punda!

MLEVI DUH!

Kuna MLEVI mmoja alikwenda kanisani ili ABATIZWE kwani alidai kuwa sasa pombe kaiacha.

Basi MCHUNGAJI akamzamisha ndani ya maji mengi na alipoibuka Mchungaji akasema,
"Nimekubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho mtakatifu,
Ulikuwa unaitwa NGONYANI sasa umekuwa JOSEPH.

MLEVI aliporudi nyumbani akaichukua CHUPA YA BIA na kuizamisha ndani ya MAJI yaliyokuwa yamejaa kwenye Ndoo, na ilipo ibuka akaiambia,

"Wewe CHUPA ulikuwa ukiitwa SAFARI LAGER na sasa Umekuwa FANTA ORANGE

KISHA AKAINYWA NA KUSEMA AMEN.