Wednesday, April 24, 2013

MAMA NA MTOTO WAKE

Mama na mtoto wake wapo kwenye taxi.Wakapita mtaa wakaona wanawake telee wamejipanga barabrani. Mtoto akaauliza "hawa nani?" mama akajibu "hao ni wake wanawasubiri waume zao watoke makazini.

 Dereve taxi akarukia "Sii umwambie mtoto ukweli. Hao ni machangudo wanauza miili yao kwa ajili ya
ngono!" Mtoto akastaajabu sana, akauliza "Dah!sasa mama kama hao badae watoto wao wanakuwa wanafannya kazi gani?"

 Mama kwa hasira akajibu "Wanakuwa madereva wa taxi!"

No comments:

Post a Comment