Friday, March 29, 2013

DOGO NOUMAA

Mtoto mmoja wa miaka sita alikuwa akilala kitanda kimoja na wazazi wake..

Siku moja akaamka usiku akapata babake yuko juu ya mama yake...mama amekunjwa miguu ikielekea kichwani.

Mtoto kuona vile akaanza kugonga godoro, 1.... 2.... 3..... Alafu akachukua mkono wa baba yake akauinua juu na kusema: "Daddie umeshinda match ila kesho mvae chupi kama wanamieleka wengine!!"

UMESHINDWA KABISA KUACHA KUJICHUA(PUNYETO)


Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo,
hawapendi hata kidogo.
Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha lakini wanashindwa.

KUJICHUA NI NINI HASA?
Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake. Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha! Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika. Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote.Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.

CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko. Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga. Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.
Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa ameshamaliza.

ATHARI ZAKE
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya
kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya 'natural’. Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika. Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo
kinapokutana na sehemu siri za kike ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza
‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake. Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!

MFADHAIKO
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili. Si ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi. Macho yanakuwa juju juu, si kwa
kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake.

KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA.
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza. Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe. Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.

KUFEDHEHEKA
Baada ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako. Hata kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko, huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna wanachopata kutoka kwa wenzao,
lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka: “Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”
Kauli hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja. Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu...halafu mwenzangu ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”
Ndugu yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza biashara zako mwenyewe. Umeona kazi hiyo?

UNATAKA KUACHA?
Hakuna dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu, NI RAHISI SANA, lakini Usitarajie kwamba nitakuja kuingia
kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu,
nitawapa dondoo chache sana.

Pitia dondoo zifuatazo;
(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)

(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.

(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.

(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.

(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.

(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na
ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA
mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha.

MAMBO 10 YANAYOPELEKEA NDOA KUVUNJIKA


1-kujifanya wajuaji wa kila kitu kwa wenza wetu

2-kujali marafiki kuliko mwenza wako wa ndani

3-kutaka matumizi makubwa kuliko uwezo,

4-uongo kwenye ndoa,,

5-kujiona uko sawa na mwenzi wako kisa tuu mnalala kitanda kimoja,,

6-kusahau wajibu wa mmoja wapo ktk ndoa,,

7-kuoana kwa sababu fulani,,,mf::pesa, umaarufu, kufuliwa na kupikiwa, mimba zisizotarajiwa

8-maneno ya watu kuyabeba bila uchunguzi,,

9-simu, fb, twitter, whatsapp n.k,,,,

10-tamaa ya macho,,,,,

WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume
wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu. Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia
moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya:
“Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la doa.Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo. Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Inashauriwa kwamba, mwanamke
anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

3. USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.

4. GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza
kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii,uwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.

5. USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana

NAMNA YAKUMNASA ANAYEKUFICHA TABIA ZAKE MBAYA.


Tatizo ambalo limekuwa likiwakuta wapenzi wengi wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wenye mwelekeo wa maisha ya ndoa ni kuingizwa ‘mkenge’ kwa kufichwa baadhi ya tabia mbaya na wapenzi wao. Wapenzi wanaoficha tabia wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuteka mapezni ya watu, lakini baadaye wakishafanisha azma yao hujiachia na kuanza kuwatesa wenzao. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanandoa wengi mpaka sasa wanajuta kufunga ndoa na wapenzi wao na kwamba kama wangetambua tabia za wenza wao mapema wasingekubali kufunga ndoa. Inawezekana hata wewe unayesoma haya unajuta kiasi cha kulalamikia mwenzako alivyobadilika tabia tofauti na mwanzo ulivyoanza kupendana naye. Hebu fuatilia dondoo hizi ili ujue namna ya kumtabua mpenzi anayekufichia makucha, ili usijiingize kwenye uhusiano usiokuwa sahihi.

MPE UHURU WA KUTOSHA.
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia simu,kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa. Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua. “Mke/mume wangu hajali mambo haya” Hujali kumbe unamteka mwisho wa yote utamnasa.

MPE MAJUKUMU
Ukisha mchagua umpendaye, huwezi kutambua uwezo wake mpaka umpe majukumu ya kufanya. Kwa mfano mtume akalipie maji,umeme au mwagize asimamie jambo fulani.Ukishafanya hivyo kaa kando mwangalie, anavyoiba chenji,anavyopunguza gharama bila kukushirikisha, lakini baadaye muulize,utashangaa alivyotibua mambo akidhani wewe si mtu wa kujali sana, kumbe ulikuwa umemtega na hatimaye umemnasa.

MUWEKE KWENYE WAKATI MGUMU
Njia nyingine ya kumnasa anayekufichia makucha ni kumweka katika wakati mgumu. Wanasema rafiki
wa kweli hujulikana kwa dhiki. Tengeneza dhiki kwa makusudi na kuzitekeleza. Akikuambia naomba
unitumie vocha mpenzi au ninunulie nguo mwambie sina pesa, halafu uone kama atakuwa na kiwango kile kile cha mapenzi. Wapo wanaume/wanawake wengine wa pesa na mishahara ya wapenzi wao, ili kuwabaini ni kuwanyima wakati mwingine.

TUMIA WATU
Katika hali ya kawaida, majirani na marafiki wanawatambua zaidi wapenzi wetu kuliko jinsi tunavyowatambua sisi. Inawezekana kabisa mpenzi wako akawa mtakatifu unapokuwepo lakini ukiondoka anajiachia ile mbaya, hivyo ili kujua tabia zake waulize rafiki na jirani zako watakusaidia kumtabua mpenzi wako.

ANGALIA ANAVYOWATENDEA WENGINE
Wapenzi wengi wanapokuwa wamepata wapenzi hutazama wanavyotendewa wao na kudhani inatosha. Mtu muungwana huwatendea wengine mema. “Aa, mama naye kanichosha kila siku anataka pesa.” Hebu sikia kauli hii, kama mtu analalamika kuchoshwa na mama yake itakuwaje kwako? Amka na kutambua kuwa anakufichia makucha na ipo siku atakubadilikia hata wewe na kukutesa. Amka usikubali kudanganywa na mpenzi mnafiki.

ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI


Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti, hutunisha misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana mapenzi unaonesha kuwa ubabe haukomeshi tabia ya usaliti. Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli.Katika hali ya kawaida usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana mume/mke. Watu huazimana magari na pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu hakusaidii, kwani ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.
Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha mpenzi wako hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea kukusaliti na kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona wameshikana mikono
mitaani kwa uhuru na raha zao. Ukiamua kuua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti upo kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali akibembelezana na‘kidume’ mwingine kwa maeneo fulani. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi msaliti.
Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa
umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu mzima endelea kunywa maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache aendelee kujiuliza mwenyewe. Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza, kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena sms hizo mkeo/ mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda na ikiwezekanaongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na umpe penzi moto
moto. Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti. Mwadhibu kwa upole, wanasaikolojia wameithibitisha
adhabu hii kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya kupiga au kukemea.Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta mwanamke/mwanaume mwingine naye akawa na tabia zile zile, ikiwa ndivyo utaacha
wangapi basi katika maisha haya? Adhabu ya mpenzi anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha
kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na hii ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia inasaidia kupunguza maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi hakusaidii.