Friday, July 27, 2012

do what is best first then follow another (opportunity cost)

Waswahili wanasema "mtaka yote hukosa yote" hasa ukizingatia kuwa na pupa na kupata mambo unayoyapenda mazuri ambayo yatakufurahisha moyo na nafsi yako. Anaepata moja zuri ni tofauti na anaekosa yote HIVYO basi usiharakie maisha, jipange na shughulikia moja basi na jengine litafuata kitaratibu..Dunia ipo kwa ajili yako haina haja ya kukimbizana nayo kwani pole pole ndio mwendo, usije ukaruka hatua (step) ukaharibu kila kitu baadae

Tuesday, July 24, 2012

Sometimes the best thing to say is nothing

Anaekaa kimya siku zote ni mshindi, ikitokea kuna pande 2 moja ipo juu ya mwenzake kwa nyenzo na mabavu njia rahisi ya huyu wa pili(mnyonge) ni kukaa kimya ni sawa na kusema "mafahari wawili hawakai zizi moja"..ikifikia wakati unaonewa na kudhulumiwa na hata kusemwa na kushirikishwa kwa ubaya katika mambo ambayo hauhusiki na ukawa umechukua hatua za kutosha ilikudhihirisha (prove your innocence) huna hatia basi vumilia na ukae kimya kwani ni moja ya njia ya kufikisha ujumbe wako.

kwa nini tunafumba macho wakati tuna sali, tunalia, tunachum na kuwaza/kuota ndoto zetu

hii yote ni kwa sababu mambo mazuri yote katika maisha hayaonekani ila tunayafeel ndani ya mtima wa moyo..usikate tamaa na ndoto zako bali amini kuna siku zitatimia na furaha ya muda mrefu ambayo ulikuwa unaisubiri inawadia

Monday, July 23, 2012

be not afraid of growing slowly, be afraid of only of standing still

pole pole ndio mwendo, ridhika na unachokipata japo kidogo..hatua uliopo sasa hivi ni tofauti na miaka mitatu iliopita hivyo basi amini kwamba miaka mitatu ijayo utakua umepiga hatua mbele.Binadamu ni tofauti na jiwe ambalo lipo vilevile (stagnant) bali binadamu anabadilika kitabia, akili na mawazo HIVYO basi usiogope kukua (kusota) taratibu katika shughuli zako bali ogopa kutofanya kabisa