Friday, May 3, 2013

TANGAZO, Mtu mwenye watoto 10 atazawadiwa mil 50;

 Jamaa baada ya kusikia tangazo akamwambia mke wake, sisi tuna watoto 9, ila nikwambie mke wangu mimi nina mtoto 1 nje ya ndoa, naomba tumchukue na huyo wawe 10 tupate hizo ml 50. Mkewe akamwambia poa. Jamaa akaenda kumfata huyo mtoto. Aliporudi hakuwaona wale 9. Akamuuliza mkewe, Watoto wako wapi? Mkewe akajibu, baba zao walipoona tangazo nao wamekuja kuchukua watoto wao, Jamaa akazimia.....!!

USINGIZI MTAMUU

Jamaa flani alikuwa amelala na mkewe.Mara akamuona mtu amesimama kitandani.
Jamaa akafoka,"Toka hapa,we ni nani mpaka unakuja kitandani mwangu?                                      " Yule mtu akajibu,"Mi ni malaika;mtakati fu petro,na hapa sio kitandani mwako uko mbinguni!"
Jamaa,"Huh! Inamaana nimekufa,mbona mi bado kijana...naomba nirudishwe!"
Malaika,"Inawez ekana lakini siwezi kukurudisha kama mtu labda urudi kama mbwa ama kuku."
Jamaa akakumbuka mbwa wanavyopata taabu ya kulinda,akaonel ea arudi kama kuku.
Malaika akamgeuza kuku,akamwambia ajifunze kutaga kabla hajapelekwa duniani.
Akachuchumaa na kuanza kujikamua;yai la kwanza likatoka.akajik amua tena,yai la pili likatoka. Akajik amua tena mara ya tatu.
Wakati yai la tatu linatoka...akas htukia amepigwa konde ikifuatwa na sauti ya hasira ya mkewe, "Pumbavu! Balaa gani hii....unakunya kitandani!

HAHAHAHA KAMA NI WEWE UNGEFANYA NINI?

Jamaa mmoja alipata mchumba akaona ni vyema amtambulishe kwa baba yake, mzee alipomuona tu akasema, "oho huyu ni dada yako ni mtoto wangu huyu nilizaa kipindi niko shule", jamaa akatafuta mchumba mwingine akafanya vile vile lakini mzee akasema "oho ulimufahamu vipi huyu ni dada yako pia" jamaa akaona isiwe shida akatafuta kimwana mwingine, digi alipopelekewa na huyo akasema "aha sasa ww mtoto kwanini unakuwa unakutana na dada zako tu, huyu naye ni dada yako tafuta mwingine ila usimwambie mama yako maana hajui kama nina watoto hawa", 
jamaa akawa na hasira sana akaenda kumpatia story yote mama yake, mama akamwambia "aha hata usijali hao sio dada zako hata kwa damu maana hata wewe huyu sio baba yako ila usimwambie maana hajui ni siri yangu ya muda mrefu, wewe fanya kuchangua unayempenda kati ya hao uoe.

UROHO M-BAYA..

Mwizi alibomoa nyumba akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye kibakuli vilivyokauka,akaonja kimoja akaona ni kitamu kina chumvi chumvi! Akafurahi akakaa chini akala vyote alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa CHUMBA CHA KUTAHIRIA!! eti unahisi alikula nini?

KWA KUPENDA SIFA.

Wahaya kwa kupenda sifa! leo katika matangazo ya vifo , ndugu Deus Rweyemamu wa masaki anasikitika kutangaza kifo cha mwanawe Joseph Rweyemamu wa Oysterbay, kilichotokea jana Australia baada ya kupaliwa na baga akiwa anaendesha hummer yake mpya. Msiba utafanyika kwa anti yake marekani, taarifa zimfikie Ronaldo Rweyemamu wa Portugal, Koku Kardashian Rweyemamu wa U.S.A, Torres Rweyemamu wa Spain, Walcot Rweyemama wa England, na house girl wao alioko Dubay katika shoping ya mwezi, akamalizia tutawasiliana baadayeeee.

ZIMA MZIKI

Jamaa alipanda tax akamwambia dereva, zima mziki dini hairuhusu kuckliza nyimbo za kidunia kwa sababu wakati wa Yesu hapakuwa na redio, dereva akatii akazma halaf akasimamisha gari na kufungua mlango wa abiria. Jamaa akamuuliza Nini tena? Dereva akajbu 'wakati wa Yesu hakukuwa na tax shuka usubiri punda!

MLEVI DUH!

Kuna MLEVI mmoja alikwenda kanisani ili ABATIZWE kwani alidai kuwa sasa pombe kaiacha.

Basi MCHUNGAJI akamzamisha ndani ya maji mengi na alipoibuka Mchungaji akasema,
"Nimekubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho mtakatifu,
Ulikuwa unaitwa NGONYANI sasa umekuwa JOSEPH.

MLEVI aliporudi nyumbani akaichukua CHUPA YA BIA na kuizamisha ndani ya MAJI yaliyokuwa yamejaa kwenye Ndoo, na ilipo ibuka akaiambia,

"Wewe CHUPA ulikuwa ukiitwa SAFARI LAGER na sasa Umekuwa FANTA ORANGE

KISHA AKAINYWA NA KUSEMA AMEN.

SOKWE MTU

Iltokea mitaa ya kati,Mwanaume mmoja alienda kuomba kazi kwenye ZOO,akaambiwa nafasiya kazi ipo lakin hakuna sokwe;hivyo utajifanya sokwe na tutakupa ngozi utavaa.Jamaa siku ya kwanza akavaa walipokuja watalii mambo yalienda vizuri.Siku iliyofuata banda lake liliwekwa juu,jamaa katika kuongeza mbwembwe kwenye kazi yake akawa anarukaruka,kwa bahati mbaya si akaanguka ndani ya banda la simba akawa anapiga kelele;mamaa nakufaaaaaa;Mara yule simba akamwambia "Acha kelele mimi mwenyewe kama wewe,rudi kwenye banda lako haraka kabla watalii hawajaja!!!!!!!!

MLEVI NA MKEWE

Mlevi alimuamsha mkewe usiku amsindikize chooni ili akajisaidie,
Mke akakataa akaondoka mwenyewe,
Aliporejea akaanza kumuhadithia mkewe maajabu aliyoyaona chooni, mkewangu choo chetu kinamaajabu siku hizi,
mke akauliza maajabu gani?
akajibu nilipofungua mlango wa chooni taa imewaka yenyewe kisha kakanipuliza kaubaridi nikajisikia rahaaa na nilipoufunga taa ikazima na kaubaridi kakaisha, mke akasema ''nyoooo mshenzi mkubwa wewe, umeshajisaidia ndani ya friji.

YUPI ANAJUA KUUCHUNA KATI YA HAWA?

Juha:Nilimpigia cm mke wangu akapokea hakusema (hallow)nikauchuna sikuongea mpaka pesa zote zikaisha!
Zoba:iligonga mlango mke wangu hakufungua,hakuniambia karibu nikasimama palepale mpaka kesho yake nikageuza nikaondoka.
Zuzu:Tangu nimuoe mke wangu hajaniita mpenz,nimegoma kulala nae hadi leo miaka 6.Wote wakamwambia we muongo,mbona una watoto wawili?Zuzu akajibu:Mpaka leo sijamuuliza watoto ni wa nani?NIMEUCHUNA TU!!!

FAMILA YA KICHAGA

Mtoto alikwenda kwa mama yake kupeleka malalamiko kwa kile alichotendewa na baba yake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Mtoto; Jana nilikwenda kumuomba baba hela ya kusuka akaninyoa nywele {kipara},
Mama; Unabahati sana lau kama ungeomba hela ya whitedent angelikung'oa meno. Lau kama mtoto angelimuomba hela ya wembe wa kukatia kucha unadhani ingelitokea nini?

BALAA LA WATOTO WA CHEKECHEA

Hebu niambie ingekua wewe ni mwalimu wa chekechea halafu vitoto viwili vya chekechea, cha kike na cha kiume vikaja kukuuliza, eti mwalimu, watoto kama sisi tunaweza kupata ujauzito? ''Ukajibu haiwezekani''. Kakiume kikamgeukia mwenzake kakamwambia si nilikuambia usiwe na wasiwasi!!!!! Ungefanyaje?

BARUA YA CHIZI

Jamaa kamkuta chizi anaandika barua .........
JAMAAA; Vp unaituma kwa nani hiyo barua?
CHIZI; Najitumia mwenyewe.
JAMAA; Kwahiyo barua inaujumbe gani?
CHIZI; He! we chizi nn, mimi nitajuajee wakati haijanifikia?

MWALIMU ALIKUTANA NA CHANGAMOTO KAMA SIO CHANGA LA MOTO!

MWALIMU; which crops do we export to euro?
MWANAFUNZI; coffee,
MWALIMU; good, how many types of coffee do we have?
MWANAFUNZI; two types,
MWLIMU; excellent boy! and what are they?
MWANAFUNZI; Coffee Anan and Coffee Olomide,
MWALIMU; safi safi sanaaa, nakuacha cha hivyo hivyo mpaka serikali iniongeze mshahara,!!!!!!!

KIFAA CHA KUKAMATA WEZI

Wamarekani walitengeneza matchine maalum kwa ajili ya kukamatia WIZI, kutokana na mafanikio iliyoyapata kule Amerika wakaamua kuipeleka Urusi, Ndani ya siku 1 ikaonesha wizi 120, wakapeleka na Ghana ndani ya masaa 3 ikabaini wizi 1000,, iliopelekwa China kwa masaa 6 ilifanikisha kukamtwa wizi 2500, Sasa kivumbi iliyoletwa Tanzania, ndani ya robo saa tu Matchine ikaibiwa yenyewe.

JAMAA ALIDONDOKA BANK

Jamaa mmoja alidondoka benk, na haikujulikana ni ni kitu gani kilichomsibu. Watu wakaanza kusema , ''mmwagie maji, mpeni maji, mpeni maji mengi''. Jamaa baada ya kuckia hivyo akaamka akasema ''nyie vp, kama ningelilitaka maji si ningelilianguka idara ya maji, kwani cpajui, hapa nipeni hela tu nyingi, ndo mana nimeangukia hapa benki'' watu mbavu hoi.

MWALIMU ALIKUTANA NA CHANGAMOTO KAMA SIO CHANGA LA MOTO!

MWALIMU; which crops do we export to euro?
MWANAFUNZI; coffee,
MWALIMU; good, how many types of coffee do we have?
MWANAFUNZI; two types,
MWLIMU; excellent boy! and what are they?
MWANAFUNZI; Coffee Anan and Coffee Olomide,
MWALIMU; safi safi sanaaa, nakuacha cha hivyo hivyo mpaka serikali iniongeze mshahara,!!!!!!!

NDANI YA DALADALA''

DEMU;samahani kaka naomba unipakate,
JAMAA; usijali njoo tu nikupakate,
DEMU; haya,
JAMAA; wewe unaonekana ni secretary?
DEMU;ndio, kwani vipi?
JAMAA; vidole vyako laini kweli!
DEMU; asante, nawewe ni fundi magari?
JAMAA; ndio, umejuaje?
DEMU; naona hapa nilipo kaa nainuliwa na kitu kama jeki!
JAMAA; hapana nadhani itakuwa mabonde tu.

MTOTO NA PESA

MTOTO ALIMUULIZA BABA YAKE,
ETI BABA UKIKUTA NOTI YA SHILINGI ELFU KUMI{10,000} NA ELFU TANO {5,000} UTAOKOTA IPI?
BABA; WEMJINGA KWELI NITAOKOTA YA ELFU KUMI {10,000}
MTOTO; WEWE NDIO MJINGA BABA MIMI NITAOKOTA ZOTE.

MCHAGA MSAFIRI

Mchaga 1 alikuwa anasafiri kwenda nje ya nchi, akaita tax impeleke airport akauliza: shngapi kwenda airport, dreva: elfu 30 tu, mchaga: jumla na mzigo itakuwa shngap, dreva: mizgo ni bure, mchaga: basi beba mizgo yangu utangulie nayo mi napanda daladala.!

OPERATION YA MACHO

Jamaa mmoja alifanyiwa operation ya macho baada ya cku 3 akawekewa macho ya paka.Doctor;vp unaona vizuri?Jamaa;NAONA PANYA TU!!!

TAFAKARI NDIO WEWE

Jamaa mmoja alikua amekaa bar akaitazama bia yake kwa zaid ya dakika 20. Akatokea jamaa mmoja baunsa mtemi akaichukua akainywa yote ile bia

jamaa akaanza kulia hata hvo baunsa akamwambia

"usilie bana nilikua nakutania tu nitakununulia nyingine"
...
jamaa akajibu

"hilo sio tatizo ila leo ninamikosi tu, asubuhi kazini nimefukuzwa, baada ya kutoka nje nkakuta gari yangu imeibiwa nikaja zangu bar , nimenunua bia yangu na kuiweka sumu ili nijiue wewe tena umeinywa"

Thursday, May 2, 2013

MUME NA MKE

Mume: Hello baby!
Mke: Hello sweety!
Mume: Nitachelewa kurud leo
Mke: Nishajua uko kwa vijanamke
vyako, ww ni malaya sana cjui ilikuaje ukanioa nakuchukia kama nn? ckupend! ckupend!
Mume: Niko BENKI hapa
Mke: Haa! Ulijuaje kama cna hela,
nitolee laki 1 baby, nakupenda sana
kuliko roho yangu, nakutengea maji
yakuoga sweety. Ucsahau hizo pesa ninunulie na chips kuku mmwaaaa!
Mume: Ni BENKI YA KUCHANGIA DAMU
Mke: Nyoooo waambie wakutoe yote.

HIZI NI TABIA ZA MSICHANA AMBAYE AMEANZA KUKUSALITI

1 Amepunguza mawasiliano. Hi ndiyo njia pekee ya kuweka uhusiano wenu karibu kana alivyokuwa akifanya mwanzo wa mapenzi yenu lakini sasa amepunguza na aishi sababu za kuwa yupo BUSY

2 Anakukwepa kila unapotaka kuonana naye. Hawezi kuonana na wewe kwa sababu utu wa ndani humsutu na hana mapenzi na wewe tena. Hivyo atajarinu kila njia za kukukwepa, kama kusingizia ameyumwa au hana muda

3 ubinafsi. Kama mwanzo mlikuwa mkishare mambo yenu ikiwa simu na siri za maisha yeye ataanza kuweka pasword na pasword ya facebook atabadilisha.

4 hawezi kukuambia hakutaki ila atakuwa hajali uwepo wako hata ukiwepo naye.

5 ayes contact hawezi kuwa na ujasiri wa kuangalia machoni tena kwa sababu ameanza kukusaliti

6 ataanza mashindano ya kuacha kufanya vitu ambavyo vilikuwa ni jukumu lake kukufantia ila sasa atakutegea wewe umfanyiue ukimuuliza kwanini amebadilika atakujibu kwa nini wewe hunifanyii haya.

MAMBO YA KUMFANYIA MSICHANA ILI UWEZE KUMTEKA ASIKUACHE HATA KAMA HUJAMTONGOZA

1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.

2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.

3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali

4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.

5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.

6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini

7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.

8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.

9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.

10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia

KITANDA CHA KAMBA

Jamaa mmoja alikuwa anala kitanda cha KAMBA na Mkewe Na watoto wao walikuwa wanalala chini ya hicho kitanda
Siku moja Jamaa akataka mchezo
Mkewe akamwambia Watoto Bado hawajalala
Jamaa Akabisha.
Ikabidi mkewe Akubali
Jamaa alipoingiza Tu BUNDUKI ikapita kwenye Tundu la Kitanda.
Jamaa akamuuza mkewe, Imeingia?
Watoto wakajibu..
"HAIJAINGIA BABA HII HUKU CHINI"!

KITANDA CHA KAMBA

Jamaa mmoja alikuwa anala kitanda cha KAMBA na Mkewe Na watoto wao walikuwa wanalala chini ya hicho kitanda
Siku moja Jamaa akataka mchezo
Mkewe akamwambia Watoto Bado hawajalala
Jamaa Akabisha.
Ikabidi mkewe Akubali
Jamaa alipoingiza Tu BUNDUKI ikapita kwenye Tundu la Kitanda.
Jamaa akamuuza mkewe, Imeingia?
Watoto wakajibu..
"HAIJAINGIA BABA HII HUKU CHINI"!

MTOTO NA BABA

mtoto;baba nitumie hela ya matumizi huku shuleni hali mbaya la sivyo nitajinyonga
baba; huku nyumbani hali mbaya zaidi kama unajinyonga sawa tu kwasababu utapunguza bajeti. kopa kamba nitakuja kulipa nitakapokuja kuchukua mwili wako. Mungu akulaze mahali pema peponi mwanangu.

MWALIMU KASINZIA DARASANI

MWALIMU Kasinzia darasani , DOGO kamfuata na kumwambia Teacher mbona umetupa zoezi tufanye alafu unasinzia ??

[MWALIMU:] ''hapana mimi sijalala !"

[DOGO]: ''kwani hapa ulikuwa unafanya nini mda huu ? mimi nimekuona umelala''

[MWALIMU:] ''nilikuwa naongea na MUNGU!''

KESHO YAKE

DOGO kasinzia Darasana wakati kipindi linaendelea. MWALIMU akamuamsha
"DOGO, Yani unathubutu kusinzia kwenye kipindi changu?"

[DOGO:] "Hapana mwalimu sijasinzia!"

[MWALIMU:] " Enhee Tuambie Basi ulikuwa unafanya nini ? maana darasa zima limekuona"

[DOGO: ] "nilikuwa naongea na MUNGU na mimi Pia "

MWALIMU Kwa Hasira huku akipiga kelele , " Enhe Hebu Tuambie MUNGU wako Amesemaje ???!?!" maana naona watu mnatafuta Viboko Asubuhi Asubuhi.

[DOGO:] "MUNGU Kasema Hakuongea na wewe Hapo Jana !"

UROHO M-BAYA..

Mwizi alibomoa nyumba akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye kibakuli vilivyokauka,akaonja kimoja akaona ni kitamu kina chumvi chumvi! Akafurahi akakaa chini akala vyote alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa CHUMBA CHA KUTAHIRIA!! eti unahisi alikula nini?

MTALII NDANI YA BONGO

Mtalii ndani ya Bongo kaona nazi, akawa hajui nini. Akawauliza wenyeji, wakamjibu "Hilo yai la tembo!". Akataka kujua linatotoa vipi. Wakamwambia unalikalia halafu unasugua kwa matako mpaka anatoka tembo. Akarudi nchini kwao, akawambia wanae waanze kusugua. Sugua, sugua wapi! Hamna tembo. Akamwabia mkewe, sugua, sugua wapi! Akaona aingia yeye mzee wa kazi! Akawa kwa nguvu nyingi kichizi! SUGUA, SUGUA, SUGUA, mara ghafla watoto wanaanza kushangilia

"Mkonge, mkonge, mkonge..".. Mzee akazidisha nguvu, mara watoto tena

"Mashkio, Maskiooo, Mashkiooo"..
Mzee akaona bora amchungulie huyo tembo, kucheki vizuri kumbe ilikuwa suruali yake imechanika!!

JAMAA KAINGIA BAR KWA FUJO

JAMAA:lete bia hapa,na kila mmoja humu ndani mpe bia yake,maana nikinywa bia nataka kila mtu anywe bia..
WATU:Haaa..wakapewa bia
JAMAA:Lete mchemsho hapa,na kila mmoja mpe mchemsho wake,mana nikila mchemsho na kila mtu ale mchemsho
WATU:eeee..makofi kwa jamaa..muhudumu akawapa
JAMAA:leta bili hapa na kila mtu mpe bili yake mana ninapolipa bili nataka nione kila mtu analipa bili yake..
WATU: Vilio na mayowe!!

MLEVI NOMAA

Mlevi mmoja alikuwa anapita katika Mkutano wa Injili akasikia Mhubiri wa neno akisema "Msitende dhambi msije mkaenda motoni"

Mlevi akajibu "Nanyinyi huko Peponi mkipewa Mahindi Mabichi msije kuomba moto!"

CHEZEA MADENGE WEWE!

MADENGE alimuuliza MWL; Hivi ukichanganya OMO na FOMA zitatoa POVU!? MWL akajibu kwa HASIRA 'swali gani la KIPUUZI hilo, zitatoa ndio kwa SABABU zote ni SABUNI,!? MADENGE akasema: WEWE ndiyo MPUUZI na MAJIBU yako ni ya KIPUUZI!, bwege WEWE Zitatoaje POVU wakati HATUJAWEKA maji.?DAH! Mwalm hoi.!

MAJINA YA VIMADA

JINSI WANAUME WANAVYO SAVE MAJINA YA VIMADA/MPANGO KANDO KWENYE SIMU ZAO ILIKUKWEPA KUGUNDULIKA NA WAPENZI WAO

1. Mwenye Nyumba
2. Fundi wa viatu
3. Battery low
4. customer care
5. Sister
6. Binamu
7. Josef wa maziwa
8. Boss
9. Daktari wa Meno
10. missed call
11. Mama mdogo

MADENGE

Madenge ali2mwa sokoni na mama yake kununua njegere akiwa njiani anarudi na njegere moja ikadondoka ikabimbilika akasema anhaa kumbe mnajua kutembea! Akamwaga zote chini , mtanikuta nyumbani alipofika nyumbani mama yake akamuliza madenge njegere ziko wapi ? Madenge ziko njiani zinakuja !