Friday, May 3, 2013
MLEVI NA MKEWE
Mlevi alimuamsha mkewe usiku amsindikize chooni ili akajisaidie,
Mke akakataa akaondoka mwenyewe,
Aliporejea akaanza kumuhadithia mkewe maajabu aliyoyaona chooni, mkewangu choo chetu kinamaajabu siku hizi,
mke akauliza maajabu gani?
akajibu nilipofungua mlango wa chooni taa imewaka yenyewe kisha
kakanipuliza kaubaridi nikajisikia rahaaa na nilipoufunga taa ikazima na
kaubaridi kakaisha, mke akasema ''nyoooo mshenzi mkubwa wewe,
umeshajisaidia ndani ya friji.
YUPI ANAJUA KUUCHUNA KATI YA HAWA?
Juha:Nilimpigia cm mke wangu akapokea hakusema (hallow)nikauchuna sikuongea mpaka pesa zote zikaisha!
Zoba:iligonga mlango mke wangu hakufungua,hakuniambia karibu nikasimama palepale mpaka kesho yake nikageuza nikaondoka.
Zuzu:Tangu nimuoe mke wangu hajaniita mpenz,nimegoma kulala nae hadi
leo miaka 6.Wote wakamwambia we muongo,mbona una watoto wawili?Zuzu
akajibu:Mpaka leo sijamuuliza watoto ni wa nani?NIMEUCHUNA TU!!!
FAMILA YA KICHAGA
Mtoto alikwenda kwa mama yake kupeleka malalamiko kwa kile alichotendewa na baba yake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Mtoto; Jana nilikwenda kumuomba baba hela ya kusuka akaninyoa nywele {kipara},
Mama; Unabahati sana lau kama ungeomba hela ya whitedent angelikung'oa
meno. Lau kama mtoto angelimuomba hela ya wembe wa kukatia kucha
unadhani ingelitokea nini?
BALAA LA WATOTO WA CHEKECHEA
Hebu niambie ingekua wewe ni mwalimu wa chekechea halafu vitoto viwili vya chekechea, cha kike na cha kiume vikaja kukuuliza, eti mwalimu, watoto kama sisi tunaweza kupata ujauzito? ''Ukajibu haiwezekani''. Kakiume kikamgeukia mwenzake kakamwambia si nilikuambia usiwe na wasiwasi!!!!! Ungefanyaje?
BARUA YA CHIZI
Jamaa kamkuta chizi anaandika barua .........
JAMAAA; Vp unaituma kwa nani hiyo barua?
CHIZI; Najitumia mwenyewe.
JAMAA; Kwahiyo barua inaujumbe gani?
CHIZI; He! we chizi nn, mimi nitajuajee wakati haijanifikia?
MWALIMU ALIKUTANA NA CHANGAMOTO KAMA SIO CHANGA LA MOTO!
MWALIMU; which crops do we export to euro?
MWANAFUNZI; coffee,
MWALIMU; good, how many types of coffee do we have?
MWANAFUNZI; two types,
MWLIMU; excellent boy! and what are they?
MWANAFUNZI; Coffee Anan and Coffee Olomide,
MWALIMU; safi safi sanaaa, nakuacha cha hivyo hivyo mpaka serikali iniongeze mshahara,!!!!!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)