1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo
mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye
ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.
2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi
gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa
wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi
cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana
ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.
3. Busu la ghafla na
kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha
zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi
humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na
kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali
4. Tambua mahitaji
yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale
kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa
sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha
unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi.
Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi
lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au
amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa
kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.
5. Mchukue mpenzi wako
out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana
hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa
na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.
6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda
kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia
kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini
7. Ukijiona upo busy
sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama
ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha
unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.
8.
Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana
hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka
pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.
9. Epuka maugomvi
na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu
ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza
unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye
hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.
10. Mdekeze.
Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo
mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati
wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu
kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio
maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata
kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora
msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia
No comments:
Post a Comment