Friday, May 3, 2013

MLEVI DUH!

Kuna MLEVI mmoja alikwenda kanisani ili ABATIZWE kwani alidai kuwa sasa pombe kaiacha.

Basi MCHUNGAJI akamzamisha ndani ya maji mengi na alipoibuka Mchungaji akasema,
"Nimekubatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho mtakatifu,
Ulikuwa unaitwa NGONYANI sasa umekuwa JOSEPH.

MLEVI aliporudi nyumbani akaichukua CHUPA YA BIA na kuizamisha ndani ya MAJI yaliyokuwa yamejaa kwenye Ndoo, na ilipo ibuka akaiambia,

"Wewe CHUPA ulikuwa ukiitwa SAFARI LAGER na sasa Umekuwa FANTA ORANGE

KISHA AKAINYWA NA KUSEMA AMEN.

No comments:

Post a Comment