Friday, May 3, 2013

MLEVI NA MKEWE

Mlevi alimuamsha mkewe usiku amsindikize chooni ili akajisaidie,
Mke akakataa akaondoka mwenyewe,
Aliporejea akaanza kumuhadithia mkewe maajabu aliyoyaona chooni, mkewangu choo chetu kinamaajabu siku hizi,
mke akauliza maajabu gani?
akajibu nilipofungua mlango wa chooni taa imewaka yenyewe kisha kakanipuliza kaubaridi nikajisikia rahaaa na nilipoufunga taa ikazima na kaubaridi kakaisha, mke akasema ''nyoooo mshenzi mkubwa wewe, umeshajisaidia ndani ya friji.

No comments:

Post a Comment