Thursday, May 2, 2013

UROHO M-BAYA..

Mwizi alibomoa nyumba akaingia kwenye stoo akaona vinyama kwenye kibakuli vilivyokauka,akaonja kimoja akaona ni kitamu kina chumvi chumvi! Akafurahi akakaa chini akala vyote alipomaliza akaangalia juu ya mlango akaona pameandikwa CHUMBA CHA KUTAHIRIA!! eti unahisi alikula nini?

MTALII NDANI YA BONGO

Mtalii ndani ya Bongo kaona nazi, akawa hajui nini. Akawauliza wenyeji, wakamjibu "Hilo yai la tembo!". Akataka kujua linatotoa vipi. Wakamwambia unalikalia halafu unasugua kwa matako mpaka anatoka tembo. Akarudi nchini kwao, akawambia wanae waanze kusugua. Sugua, sugua wapi! Hamna tembo. Akamwabia mkewe, sugua, sugua wapi! Akaona aingia yeye mzee wa kazi! Akawa kwa nguvu nyingi kichizi! SUGUA, SUGUA, SUGUA, mara ghafla watoto wanaanza kushangilia

"Mkonge, mkonge, mkonge..".. Mzee akazidisha nguvu, mara watoto tena

"Mashkio, Maskiooo, Mashkiooo"..
Mzee akaona bora amchungulie huyo tembo, kucheki vizuri kumbe ilikuwa suruali yake imechanika!!

JAMAA KAINGIA BAR KWA FUJO

JAMAA:lete bia hapa,na kila mmoja humu ndani mpe bia yake,maana nikinywa bia nataka kila mtu anywe bia..
WATU:Haaa..wakapewa bia
JAMAA:Lete mchemsho hapa,na kila mmoja mpe mchemsho wake,mana nikila mchemsho na kila mtu ale mchemsho
WATU:eeee..makofi kwa jamaa..muhudumu akawapa
JAMAA:leta bili hapa na kila mtu mpe bili yake mana ninapolipa bili nataka nione kila mtu analipa bili yake..
WATU: Vilio na mayowe!!

MLEVI NOMAA

Mlevi mmoja alikuwa anapita katika Mkutano wa Injili akasikia Mhubiri wa neno akisema "Msitende dhambi msije mkaenda motoni"

Mlevi akajibu "Nanyinyi huko Peponi mkipewa Mahindi Mabichi msije kuomba moto!"

CHEZEA MADENGE WEWE!

MADENGE alimuuliza MWL; Hivi ukichanganya OMO na FOMA zitatoa POVU!? MWL akajibu kwa HASIRA 'swali gani la KIPUUZI hilo, zitatoa ndio kwa SABABU zote ni SABUNI,!? MADENGE akasema: WEWE ndiyo MPUUZI na MAJIBU yako ni ya KIPUUZI!, bwege WEWE Zitatoaje POVU wakati HATUJAWEKA maji.?DAH! Mwalm hoi.!

MAJINA YA VIMADA

JINSI WANAUME WANAVYO SAVE MAJINA YA VIMADA/MPANGO KANDO KWENYE SIMU ZAO ILIKUKWEPA KUGUNDULIKA NA WAPENZI WAO

1. Mwenye Nyumba
2. Fundi wa viatu
3. Battery low
4. customer care
5. Sister
6. Binamu
7. Josef wa maziwa
8. Boss
9. Daktari wa Meno
10. missed call
11. Mama mdogo

MADENGE

Madenge ali2mwa sokoni na mama yake kununua njegere akiwa njiani anarudi na njegere moja ikadondoka ikabimbilika akasema anhaa kumbe mnajua kutembea! Akamwaga zote chini , mtanikuta nyumbani alipofika nyumbani mama yake akamuliza madenge njegere ziko wapi ? Madenge ziko njiani zinakuja !