Friday, March 29, 2013

UMESHINDWA KABISA KUACHA KUJICHUA(PUNYETO)


Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo,
hawapendi hata kidogo.
Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha lakini wanashindwa.

KUJICHUA NI NINI HASA?
Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake. Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha! Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.

INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika. Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote.Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.

CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko. Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga. Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.
Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa ameshamaliza.

ATHARI ZAKE
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya
kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya 'natural’. Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika. Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo
kinapokutana na sehemu siri za kike ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza
‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake. Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!

MFADHAIKO
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili. Si ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi. Macho yanakuwa juju juu, si kwa
kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake.

KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA.
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza. Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe. Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.

KUFEDHEHEKA
Baada ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako. Hata kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko, huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna wanachopata kutoka kwa wenzao,
lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka: “Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”
Kauli hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja. Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu...halafu mwenzangu ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”
Ndugu yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza biashara zako mwenyewe. Umeona kazi hiyo?

UNATAKA KUACHA?
Hakuna dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu, NI RAHISI SANA, lakini Usitarajie kwamba nitakuja kuingia
kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu,
nitawapa dondoo chache sana.

Pitia dondoo zifuatazo;
(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)

(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.

(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.

(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.

(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.

(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na
ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA
mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha.

3 comments:

  1. Kwa ushauri na njia za kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kuangalia picha za porngraphy na kupiga punyeto au masterbation kwa vijana wenzangu na pia namna ya kurudisha nguvu za uume zilizopungua kwa tiba ya vyakula, please tuwasiline #usharinasaha18@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Kwa ushauri na njia za kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kuangalia picha za porngraphy na kupiga punyeto au masterbation kwa vijana wenzangu na pia namna ya kurudisha nguvu za uume zilizopungua kwa tiba ya vyakula, please tuwasiline #usharinasaha18@gmail.com

    ReplyDelete