HAHAHAHA KAMA NI WEWE UNGEFANYA NINI?
Jamaa
mmoja alipata mchumba akaona ni vyema amtambulishe kwa baba yake, mzee
alipomuona tu akasema, "oho huyu ni dada yako ni mtoto wangu huyu
nilizaa kipindi niko shule", jamaa akatafuta mchumba mwingine akafanya
vile vile lakini mzee akasema "oho ulimufahamu vipi huyu ni dada yako
pia" jamaa akaona isiwe shida akatafuta kimwana mwingine, digi
alipopelekewa na huyo akasema "aha sasa ww mtoto kwanini unakuwa
unakutana na dada zako tu, huyu naye ni dada yako tafuta mwingine ila
usimwambie mama yako maana hajui kama nina watoto hawa",
jamaa akawa na
hasira sana akaenda kumpatia story yote mama yake, mama akamwambia "aha
hata usijali hao sio dada zako hata kwa damu maana hata wewe huyu sio
baba yako ila usimwambie maana hajui ni siri yangu ya muda mrefu, wewe
fanya kuchangua unayempenda kati ya hao uoe.
No comments:
Post a Comment