Mtanzania, Mnyarwanda, na Mkenya walikamatwa na madawa ya kulevya
China. Wakaambiwa adhabu ni mbili kifo au adhabu nyingine ambayo
wakiishindwa pia wanauawa. Wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu
bahati yao. Wakapelekwa msituni wakaambiwa waingie msituni kila mmoja
kwa njia yake halafu kila mmoja arudi na matunda kumi ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
Mnyarwanda akarudi wa kwanza. Karudi na maepo kumi. Akaambiwa adhabu ni
kuyameza yote mazima mazima moja baada ya jingine bila kufumba macho
bila kulia wala kucheka wala kujitikisa! Akameza la kwanza. Safi. Kumeza
la pili akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Wa pili Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogoo. Kumi. Vya kufanana.
Vidogo kama pipi. Akaambiwa masharti. Akaanza kula bila kufumbua macho
wala kulia wala nini. Alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua
kicheko! Akapigwa risasi pia akafa. Wakiwa kuzimu Mnyarwanda akamuuliza
Mkenya.. "Vipi wewe mbona ulishindwa kuvumilia wakati ulibakisha kitunda
kimoja tu?" Mkenya akajibu: "Kaka, nilishindwa kuzuia kicheko maana
nilimwona Mtanzania anakuja na matikiti maji!".....
No comments:
Post a Comment