1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha
mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume
wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la
kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu. Msaada
unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si
kumwambia hawezi, bali ni kumtia
moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu
za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya:
“Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la doa.Hawajishughulishi
kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya
mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo
anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano
toka kwa mwenzake.Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni
watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa
mchezo huo. Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini
pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka
mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke
anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo,
asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi,
asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna
kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya
wapungukiwe na nguvu.
3. USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu
wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu
wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume
apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni
muhimu sana katika mapenzi.
4. GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni
gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo
yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.Mwanamke anapokuwa mwingi
wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza
kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha
kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii,uwafanya waume zao wawe na msisimko
wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
5. USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume.Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa
anasalitiwa, huumia sana
No comments:
Post a Comment